Wananchi wa kijiji cha Kwa Ugoro, Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru wameishukuru Serikali kuridhia ombi la kuwaongezea muda wa kulipia mashamba ku0wenye eneo la kijiji kutoka mradi wa Valeska kulipa ifikapo tarehe 30 Mei 2023.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara, wananchi hao wameishukuru Serikali mbali na kuwapa Hekari 500 kutoka mradi wa Shamba la Valeska ambapo kama kijiji walikubaliana watakao pata mashamba kulipia ili fedha zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo. Wameongezewa muda wa kukamilisha malipo ambao ni fursa kwao kujipanga kukamilisha malipo" Hakika tumeona Serikali hii ya awamu ya sita ilivyosikivu, tunashukuru sana kuongezewa muda wa kulipia haya Mashamba" amesema Nuhu Kitundu Mkazi wa Kwaugoro.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kichama Meru Ndewirwa Soori Mbise ametoa wito kwa Wananchi kuwa Wazalendo, Kudumisha amani na kutenda haki katika masuala ya kijamii ili kuharakisha maendeleo, ambapo amebainisha CCM itaendelea kuisimamia Serikali kuhakikisha Wananchi wanatatuliwa kero walizonazo kwa wakati, kama jitihada za kuharakisha maendeleo.
Naye, Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe alihimiza umma kufuatwa kwa Sheria, Kanuni na Taratibu katika utekelezaji wa Shughuli za Kiserikali.
kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Maroroni Mhe.Yona Nnko ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi wa Vijiji vya Kata ya Maroroni kikiwemo kijiji cha Kwaugoro ili kuiletea Kata hiyo Maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwaugoro Jackson Kivuyo ametoa wito kwa Wananchi wa Kijiji hicho waliopata Mashamba kulipia ndani ya muda ulioongezwa ili Kijiji hicho kipate fedha za kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwa manufaa ya Wananchi Wengine.
Awali,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili amesema Halmashauri hiyo itahakikisha kila fursa inakuwa na maendeleo kwa Wananchi wa Meru.
Ikumbukwe Tarehe 16 Machi 2023 wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii kutembelea na kukaguau utekelezaji Mradi wa Shamba la Valeska ambalo wananchi wa Vijiji vya Kwaugoro, Valeska na Maroroni walipewa Hekari 500 kila kijiji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa