Wito watolewa kwa Wazazi ,Viongozi na wataalam kufuatilia na kuhakikisha wanafunzi wote waliopangwa katika shule za Msingi na Sekondari wanaripoti Mashuleni.
Hayo yamejiri wakati wa Siku ya Kwanza ya Mkutano wa baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Madiwani wamehoji uwepo wa wanafunzi watoro katika taarifa za utekelezaji za Kata .
Mhe.Glory Kaaya ambaye ni Diwani Viti maalum Tarafa ya Mbuguni amesema kunahaja ya Halmashauri kuongezwa jitihada kukomesha utoro mashuleni kwani taarifa za Kata zinaonesha kumekuwa na Wanafunzi watoro zaidi ya 100.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Jeremia Kishili amewaagiza wataalam kufuatilia taarifa hiyo ili kubaini uhalisia wake kwani baadhi ya Wanafunzi wanaosemekana ni watoro wapo katika Shule za Binafsi .
Kishili ametoa Wito kwa Wazazi ,Viongozi wakiwemo Waheshimiwa Madiwani kushiriki kikamilifu kutokomeza hali ya utoro mashuleni.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga amesema zoezi la kuwabaini wanafunzi ambao hawajaripoti mashuleni linaendelea.
Mkutano huo wa baraza kwa kipindi cha Januari hadi Machi wa Siku 2 umekamilika kwa siku ya kwanza ambapo miongoni kwa agenda zake ni uwasilishaji wa taarifa za Kata.
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza (ishara ya Mkono)wakati wa Mkutano wa Baraza la Halmashauri hiyo. Kulia kwake , ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga, Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri akifuatiwa na Karibu Tawala Wilaya ya Arumeru.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano wa Baraza .
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano wa Baraza .
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano wa Baraza .
Wataalum wakati wa Mkutano wa Baraza .
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano wa Baraza .
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano wa Baraza .
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano wa Baraza .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa