Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii, mapema leo hii imefanya hafla ya kuadhimisha siku ya Vijana Duniani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa DSW Shirika lisilo la kiserikali linalopatikana Tengeru. Aidha katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi Mgeni rasmi alipata wasaa wakuhudhuria na kuzungumza na Vijana.
Kupitia hafla hiyo Mhe. Mwinyi ametoa pongezi kwa taasisi zote zinazotoa huduma kuhusu vijana na kuwapongeza vijana wote walioweza kuonyesha bidhaa zao na namna wanavyotumia taaluma zao kujikwamua katika Wimbledon la ukosefu wa ajira
Aidha amewataka vijana na Taasisi zote kuwa staring wa mbele katika kupambana na unyanyasaji wa kijinsia jambo ambalo hupelekea kuleta changamoto kubwa kwa vijana wengi wakike na wakiume na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kupinga swala hilo
Mwisho Mhe. Mwinyi amewataka vijana kuchangamkia fursa zote zinazokuja katika maeneo yao jambo ambalo litafanya kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na mwisho uchumi wa jumla na kuleta maendeleo katika Taifa letu