Waziri Mkuu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezungumza na hadhara ya wafanyakazi waliokusanyika kushiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani mkoani Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, tarehe 01, Mei, 2024.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa, siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ni siku maalum kwa ajili ya wafanyakazi kutafakari na kutathmini namna walivyotekeleza majukumu yao, kwa kuzingatia malengo waliyojiwekea katika mwaka husika.
Amesema kuwa siku hiyo inatoa fursa kwa wafanyakazi wote duniani kuweka mipango kwa ajili ya mwaka unaofuata na ndiyo maana inafanyika kipindi ambacho nchini nyingi duniani zinakuwa katika maandalizi ya Bajeti.
“Siku hii muhimu inatukumbusha wajibu wetu wafanyakazi wa kujadiliana kwa pamoja changamoto zilizopo katika utendaji wetu wa kazi na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja na hatimaye kuleta tija katika maeneo ya kazi”. Amesema Majaliwa .
Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza watumishi wote kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwaletea watanzania maendeleo. “Sisi sote ni mashahidi wa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na kijamii.
Aidha, katika Maadhimisho hayo, Mgeni Rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa