Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na mlezi wa CCM Arusha,Rajabu Abdallah,ameongoza mamia ya wafuasi wa chama hicho katika maadhimisho ya miaka 48 ya CCM ngazi ya mkoa.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Jumanne Januari 4,2025 katika Viwanja vya Soko la Tengeru,Kata ya Akheri wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha.
Rajabu akiongozana na viongozi mbalimbali wa CCM kutoka Wilaya zote saba za Mkoa wa Arusha,wakiwemo wabunge,ameanza kwa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Meru iliyopo katika Halmashauri ya Meru Kata ya Akheri.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa