Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ametoa wito kwa Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali kushirikiana na Halmashauri hiyo katika maswala mbalimbali ya maendeleo " tunashukuru Mashirika mbali mbali likiwemo Shirika la DSW kwa Kushirikiana nasi wakati wa mlipuko wa UVIKO-19 sambamba na kuhamasisha juu ya Afya ya uzazi ,niwakaribishe wadau wa maendeleo na Mashirika kushirikiana na Halmashauri katika maswala mbalimbali ya kimaendeleo "amesema Makwinya .
Mwl.Makwinya amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya kujitolea Duniani yenye Kauli mbiu ya "kujitolea kwa ajili ya mustakabali wa pamoja " yanayofanywa na Shirika la DSW kwa Kushirikiana na UNV .
Maadhimisho hayo yanayoendelea katika Makao Makuu ya DSW na hufanyika kila Mwaka tarehe 5 Desemba, ambapo kwa Mwaka huu yanalenga kuhamasisha Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Asasi za Kiraia na Serikali kwa ujumla kujitole ili kudumisha amani, maendeleo ya Kitaifa na Kimataifa , yenye Kauli mbiu ya "JITOLEE SASA KWAAJILI YA MUSTAKABALI WA PAMOJA" .
Aidha, Mgeni Rasmi ni Balozi wa Uganda NchiniTanzania Richard Kabonero.
Ikumbukwe, Siku ya kimataifa ya kujitolea ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia azimio la tarehe 1 Desemba 1985 na kwa mujibu wa Shirika la kujitolea la Umoja wa Mataifa zaidi ya watu Bilioni Moja hujitolea Duniani Kote.
Aidha Kazi nyingi za kujitolea sio rasmi kwani karibu asilimia 70%ya watu wanaojitolea wanafanya Kazi katika jumuia zao ili kuwasaidia watu wanaowazunguka.
Mwl.Zainabu Makwinya ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea Duniani.
Meza Kuu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya kujitolea Duniani
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa