Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru imefanya Ziara ya kukagua ujenzi wa Madarasa Manne yanayojengwa katika shule ya Sekondari Imbaseni iliyopo Kata ya Imbaseni.
Shule hiyo imepokea fedha kutoka Serikali Kuu shilingi Milioni 50 tarehe 3 Aprili 2024 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vinne vya madarasa vilivyokuwa vimejengwa kwa nguvu za wananchi.
Ujenzi wa madarasa hayo, Madarasa mawili na ofisi yapo tayari na yanatumika lakini madarasa mawili na ofisi upande wa pili yapo hatua ya ukamilishaji.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Felister Nanyaro amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Imbaseni Mhe. Jeremia Kishili kwa ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa katika Kata yake.
Ukaguzi huo ni utaratibu wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa