Mheshiwa Jeremia Kishili, Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru ametoa wito kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo kushirikiana ili kuwaletea Maendeleo Wananchi "Wananchi wanahitaji miundombinu mizuri ya barabara, huduma bora za afya na maji hivyo hatuna budi kushirikiana na Mhe.Mbunge, Menejimenti pamoja na wadau kuharakisha maendeleo ya Meru ." amesisitiza Mhe. Kishili.
Hayo yamejiri wakati wa Mkutano wa kwanza wa Baraza jipya la Halmashauri ambapo Waheshimiwa Madiwani 36 wamekula kiapo cha udiwani na kutoa Tamko la Maadili kuanza kazi rasmi.
Kiapo hicho kimeongozwa na Hakimu mkazi wa Mahakama ya mwanzo Maji ya Chai Mhe .Walter Mwijage na kimewajumuisha Madiwani 36 ambapo kati yao madiwani 9
ni wa Viti Maalumu na mmoja ni Mhe. Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Aidha, Mhe.Kishili alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kupata kura za wajumbe wote 36. Kwa upande mwingine, Mheshimiwa Felister Nanyaro alichaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kura za ndio za wajumbe wote. Viongozi hawa wamewashukuru wajumbe kwa kuwaamini na kuahidi kushirikiana nao kuijenga Meru yenye Maendeleo.
Mhe. Dkt.John D. Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki amesema katika kutatua changamoto kubwa ya barabara zisizopitika kirahisi Halmashauri inapaswa kuimirasha usimamizi wa Mitambo yake kwa kuhakikisha shughuli zote za mitambo hiyo zinaratibiwa na Halmashauri yenyewe.
Aidha ,wajumbe walipongeza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa kipindi ambacho Halmashauri haikuwa na Madiwani. Taarifa hiyo iliwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Emmanuel J. Mkongo .
Aidha, Baraza za Halmashauri lilitekeleza jukumu la uundaji wa Kamati za Kudumu za Halmashauri hiyo kwa kuwachagua Wenyeviti wa Kamati hizo Mheshimiwa Jeremia J. Kishili-Kamati ya Fedha , Utawala na Mipango, Mhe.Lucas Kaaya Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira na Mhe. Kaanael Ayo Kamati ya Elimu ,Afya na Maji.
Ikumbukwe Waheshimiwa Madiwani wote 35 na Mbunge wanatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Bi. Felister Nanyaro makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akila kiapo cha Udiwani.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt.John D. Pallangyo akitoa tamko la maadili (kwa mujibu wa Sheria Mbunge ni diwani katika Baraza la Halmashauri)
Baadhi ya Madiwani wakitoa tamko la Maadili.
Baadhi ya Madiwani wakitoa tamko la Maadili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Emmanuel J. Mkongo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kipindi Madiwani hawakuwepo.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki akishauri kuhusiana na Mitambo ya Halmashauri wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Baadhi ya viongozi wa CCM wakati wa Mkutano.
Wakuu wa Idara,na Watumishi wa Halmashauri wakati wa Mkutano.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Mkutano.
(kulia )Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru (katikati )Makamu Mwenyekiti Mhe.Felister Nanyaro ,kushoto ni Mhe.Mbunge John Pallangyo.
Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru ,Makamu Mwenyekiti Mhe.Felister Nanyaro ,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa