Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili mapema hii Leo ameongoza Baraza la Madiwani lililokuwa limebeba ajenda Kuu ya kusikiliza na kupokea Taarifa za utekelezaji za Kata Kwa kipindi cha Oktoba-Disemba 2024.
Aidha Mhe. Kishili amewataka Madiwani kuendelea kufanya kazi yakuwasikiliza Wananchi na kushirikiana na Watendaji katika kutatua migogoro na matatizo yanayowakumba Wananchi katika Maeneo yao, aidha Mhe. Kishili Amesema kuwa hataki kusikia swala la mfumo kuwa kikwazo chakutotoa huduma au utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Jamii.
Katika Baraza hilo Katibu wa kikao hiko ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru amewataka Watendaji kuhakikisha wanatembelea Miradi kwa lengo la kufanya ukaguzi wakati Miradi inatekelezwa nakuacha tabia yakusubiri wataalamu mpaka wafike kwenye Maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa