Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri hiyo amemkaribisha Mwl.Zainabu J. Makwinya ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Mhe.Kishili amesema swala la maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ni kipaombele cha Madiwani wa Halmashauri hiyo hivyo watashirikiana kikamilifu na Mkurugenzi Mwl.Zainabu kuijenga Meru.
Kishili amtaka Bw.Emmanuel John Mkongo ambaye amepangwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, kuendelea kuchapa Kazi kwa juhudi; viwango, weledi na uadilifu kama alivyofanya Meru .
*KAZI IENDELEE*
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili na Mwl.Zainabu J. Makwinya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa