Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitoa sh. Milioni 900 za ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, Bohari ya Dawa, kichomea taka cha kisasa pamoja na ukarabati wa majengo ya zamani katika Hospitali ya Wilaya ya Meru iliyopo Kata ya ya Akheri.
Leo tarehe 22 Oktoba, 2024 Waheshimiwa Madiwani na Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamefanya ziara na kukagua ujenzi wa mradi huo. Ukaguzi huo ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa Miradi kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba 2024 kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Wajumbe hao baada ya kukagua mradi huo wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kutoa pongezi kubwa kwa Kamati ya Ujenzi, Diwani wa Kata ya Akheri Mhe. Julius Mungure na kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya kwa usimamizi mzuri na kwa kazi nzuri.
Pia, wajumbe walikagua jengo lililokarabatiwa la watoto Njiti ambapo lilipokea sh. Milioni 25 kutoka Serikali kuu kupitia wafadhili na kwa mwaka Wa Fedha 204/2025 hospitali imepokea Fedha sh. Milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya hospitali hiyo.
Aidha, kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani Husna Maganga Mhe. Diwani Vitimaalum Tarafa ya Mbuguni amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha hizo za utekelezaji wa mradi huo.
" Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa