Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru waaswa kuzingatia tamko la maadili ili kutekeleza majukuumu yao kwa maslahi mapana ya Halmashauri.
Rai hiyo imetolewa na Afisa kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi, Ndg. Baraka Mgimba wakati wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambayo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Afisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndg.Moses Mabula amesema katika kufanya maamuzi na kutoa maagizo Madiwani wanapaswa kuzingatia Sera, Sheria ,Kanuni na Taratibu na Miongozo ili kuleta tija katika swala zima la maendele ya Halmashauri.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Emmanuel J. Mkongo amesema kuna Umuhimu mkubwa kwa Madiwani kurejea mafunzo hayo ili kufanya maamuzi na kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheriana Kanuni.
Aidha, katika semina hiyo elekezi mada za Majukumu ya Diwani, Maadili ya Viongozi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo,uendeshaji wa Vikao vya Halmashauri , Manunuzi
ya umma na matumizi ya fedha za Umma zilitolewa.
Afisa kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi, Ndg. Baraka Mgimba akitoa mafunzo wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
katikati ni Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bi. Felister Nanyaro, Kushoto mwa Makamu ni Mhe.John D. Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,kulia mwa Mwenyekiti ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo,kulia mwa Mkurugenzi ni Mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Ndg. Anacleth Mshashu.
Afisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndg.Moses Mabula akizungu wakati wa Semina.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Jonathan Kiama akizungumza wakati wa Semina kwa Madiwani .
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Mkuu wa Idara ya Utawala na rasilimali watu, Bi. Grace Mbilinyi akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Julius Ndyanabo Akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Mkuu wa Idara ya Mipango Ndg.Maarufu Mlwaya akizungumza wakati wa Semina kwa Madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa mafunzo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa