Na Annamaria Makweba
Waheshimiwa Madiwani na Wataalam katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamepatiwa mafunzo ya Utawala Bora na Afya ya Akili yatakayowawezesha kuboresha utendaji kazi katika majukumu yao ya kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amefungua mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Gateway iliyopo katika Wilaya hiyo ikiwa na lengo la kufanya tathmini kwa kazi zilizofanyika kwa mwaka katika Wilaya hiyo.
Mhe. Kaganda amewataka Wahe. Madiwani na Wataalam kujipima katika maeneo yao na kujifanyia tathmini kama wamefikia malengo katika kutoa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru, Mwl. Zainabu J. Makwinya ameeleza kuwa lengo la mafunzo haya ni kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali tunazokutana nazo tunapokuwa kazini, nje ya kazi na nyumbani.
"Tumeona ni vyema kumleta daktari wa masuala ya Saikolojia na Mkufunzi wa Masuala ya Afya ya Akili ili tuweze kupata elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto katika maisha yetu lakini pia kuboresha utendaji kazi katika maeneo yetu" alisema Makwinya.
Wakufunzi walioshiriki kutoa Mafunzo ni pamoja na Daktari wa masuala ya Saikologia na Afya ya Akili Darvin Kweka, Jackson E. Muhoho na Yona William Kitūa Wahadhiri kutoka Taasisi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa