Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wametakiwa kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri ili kutatua matatizo yanayoikabili jamii ikiwemo suala la maji,miundombinu ya barabara pamoja na elimu,hayo yameelezwa na Diwani wa kata ya Ngarinanyuki Zakaria Nko amesema kuwa ili halmashauri iweze kupata maendeleo stahiki ni vyema madiwani wakafanya kazi zao na kutumia ushauri wa kitaalamu katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayoendesha na serikali na hata ile ya wafadhili
naye diwani wa kata ya Nkuaranga Zephania Mwanuo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Maji akizungumza katika kikao cha siku tatu cha Baraza la Madiwani kilichojadili taarifa za maendeleo ya kata na kufanya uchaguzi wa kamati mbali mbali za afya,elimu,fedha na ujenzi ambapo amesema kuwa ushirikiano huo na wataalamu utazaa matunda na kuleta matokeo yanayotarajiwa na wananchi katyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Willy Njau amesema kuwa katika kikao hicho wamepokea taarifa za maendeleo za kata 8 ambapo zimewasilisha katika mahojiano na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Willy Njau amesema kuwa katika kikao hicho wamepokea taarifa za maendeleo za kata 8 ambapo zimewasilisha changamoto zinazowakabili na kutoa mapendekezo juu ya namna ya kutatua changamoto hizo ili kuleta maendeleo katika kata zao
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa