Akiongea na wandishi wa habari tarehe 23 Juni 2017 Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Meru ndg,Edward Chitete amethibitisha kupokea barua za kujiuzulu kwa waheshimiwa madiwani wanne Walio andika barua ya kujiuzulu nafasi zao ikiwa ni pamoja na kujivua uanachama wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Madiwani hao ambao ni Bryson Issangya diwani kata ya Maroroni, Emmanuel Mollel diwani kata ya Makiba,Josephine A. Mshiu diwani viti maalumu kupitia tarafa ya King'ori na Underson E.Sikawa diwani kata ya Leguruki.
Kupitia barua hizo madiwani hao wameeleza wamefikia uamuzi huo ili kujipa muda wa kufanya majukumu mengine binafsi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa