Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru mwalimu Zainabu J. Makwinya na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jeremia Kishili wamepatiwa zawadi na Waheshimiwa Madiwani Wanawake kwa usimamizi mzuri na uendeshaji wa Shughuli za Hamashauri.
Pongezi hizo wamezitoa leo katika ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri kabla ya kuingia kwenye Mkutano wa baraza la Halmashauri.
kwa niaba, ya Waheshimiwa Madiwani Wanawake, Mhe. Lukumbe Ndossi Diwani Kata ya Malula amesema kuwa wamefurahishwa na utendaji kazi na ushirikiano uliopo kati ya Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watendaji wa Halmashauri.
"Leo tumeona tuwafanyie 'suprise' Mwenyekiti na Mkurugenzi wetu kwa jinsi wanavyosukuma gurudumu la maendeleo katika Halmashauri yetu. Pia, tumeona tuwapongeze kwa kusimamia Vizuri mapato ya Halmashuri hadi kupelekea kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2022/2023." amesema Lukumbe.
Aidha, ameeleza kuwa ushirikiano wao ndio unaoleta mafanikio yanayoonekana katika Halmashauri ya Meru kwani wamekuwa wakiwashirikisha Waheshimiwa Madiwani masuala yote muhimu yanayohitaji maamuzi na utekelezaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa