Madiwani watano walioshinda kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru uliofanyika tarehe 26 Novemba 2017 waapishwa na kuungana na madiwani wenzao kwenye Mkutano wa Baraza la Halmashauri hiyo uliokua unaendelea.
Madiwani hao watokanao na chama cha mapinduzi (ccm) ambao ni Mhe. Diwani kata ya Makiba Samson Paul Laizer ,Mhe diwani kata ya Ngabobo Solomon lorgos Laizer,Mhe. Diwani Kata ya Maroroni Yona Ndelekwa Kaaya , Mhe. Diwani kata ya Ambureni Japheti Joseph Jackson na Mhe. Diwani wa Kata ya Leguruki Anderson Elisa Kaaya wamekaribishwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Will j. Njau rasmi kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kama wajumbe halali baada ya taratibu za kuapishwa zilizoongozwa na Mwanasheria wa Halmashauri ya hiyo, Wakili na kamishina wa viapo Magdalena Olesiiyai John.
Aidha Mkutano huo wa siku 2 umekamilika kwa siku ya kwaza kwa kupokea na kujadili taarifa za kata kwa siku ya kesho itakua ni kupokea nakujadili taarifa za kamati mbalimbali za Halmashauri hiyo.
PICHA ZA TUKIO
Madiwani wateule wakitoa tamko la Uadilifu wa Kiongozi wa Umma.
Mhe. Diwani kata ya Ambureni Japheti Joseph Jackson wakati akila kiapo cha Diwani
Mhe. Diwani wa Kata ya Leguruki Anderson Elisa wakati akila kiapo cha Diwani
Mhe diwani kata ya Ngabobo Solomon lorgos Laizer wakati akila kiapo cha Diwani
Mhe. Diwani kata ya Makiba Samson Paul Laizer wakati akila kiapo cha Diwani.
Mhe. Diwani Kata ya Maroroni Yona Ndelekwa Kaaya wakati akila kiapo cha Diwani
Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri Willy J. Njau akimkabidhi Mhe diwani kata ya Ngabobo Solomon lorgos Laizer nyenzo mbalimbali zikiwemo Kanuni za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Kanuni za maadili ya madiwani mara baada ya kuapishwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Willy J. Njau akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Halmashauri hiyo
Wajumbe wakifuatilia zoezi la kuapishwa kwa Madiwani
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa