Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya mapema hii Leo ametoa maelekezo kuhusu utaratibu Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Ikiwa ni Moja ya mchakato Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Aidha miongoni mwa maelekezo yaliyotolewa na Mwl. Makwinya ni Pamoja na Siku ya Uchaguzi, Muda na sehemu yakuandikisha wapiga Kura, Muda na mahali pakufanyia Uchaguzi , Sifa za wanaostahiki kupiga na kugombea nafasi za Uongozi, Nafasi zinazogombewa Ndani ya Serikali za Mitaa, Siku ya utoaji na urejeshwaji wa Fomu za kugombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Mitaa, Uteuzi wa Viongozi, Ukataji wa Rufaa, Siku na Utaratibu wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, n.k
Aidha Mwl. Makwinya ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza katika kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa kufuata kanuni na taratibu zilizotolewa ili kuhimiza maendeleo ya Halmashauri na Taifa Kwa Ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa