• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

170 WAPATA AJIRA WAKATI WA UFUNGAJI MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA ARUMERU.

Imewekwa: October 16th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg. Jerry Muro amefunga rasmi mafunzo ya  jeshi la akiba kundi 6/2020 yaliyoanza   24 februari 2020 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Akifunga mafunzo hayo, katika viwanja vya Relini, Kata ya Usa River Mkuu huyo wa Wilaya amezitaka  Taasisi na Makampuni mbalimbali yanayojishughulisha na shughuli za ulinzi Wilayani Arumeru kuhakikisha yanaajiri walinzi waliopata mafunzo ya jeshi la akiba ili kuleta tija kwenye kuimarisha ulinzi na usalama Wilayani humo.

Aidha, Muro ameipongeza timu ya jeshi la akiba Wilaya ya Arumeru  ikiongozwa na Kapteni. Issack Kimaryo kwa kuratibu mafunzo hayo kwani wahitimu wote 170 ambao wanaume ni 118 na wanawake ni 52 wameonyesha umahiri na uelewa wa hali ya juu uwanjani hapo hivyo kupelekea makampuni ya ulinzi ikiwemo Suma JKT guard, Cachson Risk management, SGA security, GB security, ADF security kuhitaji kuwaajiri Askari  wote 170 waliohitimu “fursa ya ajira ni kubwa kwani mliohitimu hamtoshi uhitaji wa Makampuni haya,natoa wito kwa vijana kujitokeza kushiriki mafunzo yanapotangazwa “amesisitiza Muro

 Akihitimisha, Muro ametoa wito kwa wahitimu hao kutumia mafunzo waliyopewa kudumisha amani na ulinzi wa raia na mali zao  sambamba na kuwa na nidhamu."Nidhamu ni dhana na silaha namba moja ya askari katika swala zima la ulinzi " amesisitiza Muro.

Mshauri wa jeshi la akiba wilaya ya Arumeru, Kapteni. Issack Kimaryo akisoma taarifa amesema kundi la 6/2020 lilianza mafunzo tarehe 24/02/2020 likiwa na wanafunzi 184  wakiwemo wanaume 124 na wanawake 60 lakini hadi kufikia tarehe ya kuhitimu wamebaki 170  ambapo 14 wameshindwa kuhitimu mafunzo kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha, Kapteni.Kimaryo amesema mafunzo hayo ya awali ya ulinzi na usalama wa umma yamechukua majuma 18 ambapo askari  walifundishwa masomo ya silaa, kwata, huduma ya kwanza, usomaji ramani, mbinu za kivita ,ujanja porini ,utimamu wa mwili na sheria za jeshi la akiba hivyo askari hao wamekidhi vigezo vyote vya jeshi la akiba  na wako tayari kulitumikia taifa katika ulinzi wa umma kwa maendeleo ya taifa na majuku mengine watakayo pangiwa katika kusaidia taasisi za umma .

Wahitimu wa mafunzo hayo Deborah ,Dorothea  mameishikuru Serikali Wilayani humu kuanzisha mafunzo hayo ambayo yamezaa matunda kwa kufungua fursa ya ajira kwa vijana pia waliweza kujifunza ukakamavu na elimu juu ya afya  .

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakifanya onesho wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji mafunzo.

Meza ya kwanza (Kulia )ni mshauri  wa jeshi la akiba wilaya ya Arumeru, Kapteni. Issack Kimaryo




Bi.Deborah akisoma risala ya wahitimu .

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akipokea risala ya wahitimu .




Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa