Wakuu wa shule za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamepatiwa Mafunzo ya ununuzi kwa kutumia njia ya kieletroniki ya NEST- "National e-procurement system of Tanzania"
Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kuanza na Wakuu wa Shule za Sekondari waliopata fedha za miradi katika shule zao.
Katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Sekondari Marcel Itambu ameeleza kuwa PPRA imeelekeza manunuzi yote kufanyika kupitia mfumo wa manunuzi ya Nest hivyo ni lazima Wakuu wa shule kupata mafunzo ya matumizi ya mfumo huo.
Aidha, Afisa Ugavi Juma Samson ameeleza kuwa mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa ngazi zote kuanzia kwa Watendaji wa Kata/Kijiji, Shule za Sekondari,Shule za Msingi, Hospitali na maendeo yote yanapotekelezwa miradi ya maendeleo ya Serikali. Bofya hapa kutazama Video https://www.instagram.com/p/C6V_BVFN5K7/
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa