• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MAFUNZO YA (MTAKUWWA )YATOLEWA KWA KAMATI YA ULINZI WA WANAWAKE/WATOTO MERU

Imewekwa: April 25th, 2018

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ( MTAKUWWA) yaliyotolewa kwa  wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Ndg. Christopher J. Kazeri amesema mafunzo hayo ni muhimu na kusisitiza kuwa wanawake na watoto mbali na kupata ulinzi wanahitaji kufahamu namna ya kujikinga/kujihami na ukatili na unyanyasaji pia amewataka wajumbe hao kufikisha mafunzo hayo kwa wengine hivyo mafunzo hayo kufikia jamii kwa upana .

Happiness Mugyabuso ambaye ni mchumi kutoka ofisi ya Waziri mkuu amesema mpango wa taifa wa miaka mitano  kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto unalengo la kuhakikisha ifikapo 2021 ukatili dhidi ya wanawake na watoto uwe umepungua kwa asilimia 50, hivyo ili kufikia lengo hilo amewasihi wajumbe kuhamasisha ,kuelimisha jamii kuacha mambo yanayo sababisha ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto na kuwa tayari kutoa msaada wa kuwanusuru na wanawake hao na watoto.

Mchumi Happiness ameeleza mpango huo  wa taifa utakapotekelezwa ipasavyo utaimarisha kipata na kuongeza idadi  ya wanawake kumiliki mambo mbalimbali ikiwemo ardhi.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la John Snow Inc (JSI)  ambalo linatekeleza mradi wa mpango wa uimarisha ji wa mfumo wa afya na ustawi wa jamii (CHSSP) unaofadhiliwa na USAID Ndg.Antony Mwendamaka amesema utekelezaji wa mradi wenye lengo linaloendana na la taifa na kimataifa  kwenye mkoa wa Arusha umetekelezwa kwenye Halmashauri mbili na kwa sasa utatekelezwa kwenye Halmashauri ya meru

Nae Afisa ustawi wa  jamii Halmashauri ya Meru Restituta Mvungi ameeleza mafunzo hayo yataongeza nguvu kwenye kutekeleza majukumu ya kitengo cha ustawi wa jamii pia amepongeza mpango wa taifa wa kupambana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ambao umeboreshwa kwani wajumbe waliopo wanauhusiano wa karibu na wanawake na watoto akituo mfano wa walimu (maafisa elimu)ambao mpango huu unawatambua kama wajumbe.

Mafunzo haya yenye lengo la  kuwawezesha wajumbe wa kamati za (MTAKUWWA) ngazi za wi kuwa na uwezo wa kuratibu afua mbalimbali kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameandaliwa na ofisi ya Raisi TAMISEMI,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee ,Wanawake na Watoto kwa kushirikia na shirika lisilo la kiserikali la JSI yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 25 Aprili hadi 27 Aprili 2018.

Ndg.Happiness Mugyabuso ambaye ni mchumi kutoka ofisi ya Waziri mkuu akieleza lengo la mradi wa taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na vijana (MTAKUWWA)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher J. Kazeri  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto yaliyotolewa kwa  wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali JSI Ndg.Antony Mwendamaka akielezea mradi (CHSSP) unaotekelezwa na shirika lake la JSI

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia kwa makini mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia kwa makini mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto

mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Patandi (jina limehifadhiwa)akifuatilia kwa makini mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Baadhi ya maafisa ustawi wa jamii wakifuatilia kwa mafunzo ya mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa