Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro ametoa wito kwa Maafisa elimu Sekondari,Wakuu wa shule za sekondari na Maafisa elimu Kata pamoja na walimu kufanya kazi kwa ushirikiano kufikia malengo ya Serikali ya kutoa elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania.
Muro ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha tathimini ya matokeo ya mtihani wa Taifa kuhitimu kidato cha nne na mtihani wa upimaji kidato cha pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kilicho wajumusisha Wakuu wa Shule 68 za Serikali na binafsi, Maafisa Elimu wa Kata 26 .
Aidha, Muro ameitaka Idara ya Elimu Sekondari na Wakuu wa Shule kuhakikisha wanafanyia kazi maazimio ya Kikao hicho ikiwa ni pamoja na kudhibiti utoro shuleni na kazini ili kuendelea kufanya vizuri kwenye Taaluma katika Halmashauri hiyo inayoshikilia nafasi ya 3 ya kitaifa katika matokeo ya kuhitimu kidato cha Nne mwaka 2020.
Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo, Mwl .Emmy Mfuru amesema asilimia ya ufaulu katika Mtihani huo wa kuhitimu kidato cha Nne imepanda kutoka 90.8 mwaka 2019 hadi 94.5 mwaka 2020 .
Mfuru amepongeza jitihada za Walimu katika ufundishaji zilizopelelea Halmashauri hiyo kutetea nafasi ya 3 kitaifa kwa miaka 2 mfululizo katika matokeo ya kuhitimu kidato cha nne na kuahidi kufanya ufuatiliaji wa maazimio ya kikao hicho.
Ndg.Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amewapongeza walimu wa shule zilizo fanya vizuri na kusisitiza umuhimu wa walimu kushirikiana "Ushirikiano ni sehemu ya mafanikio , mwalimu akiwa na amani na utulivu atafanya kazi yake kwa bidii na ufanisi mkubwa"amesisitiza Mkongo.
Mkongo ametoa wito kwa Walimu kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wanafunzi kupenda na kusoma masomo ya Sayansi kwa kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kusoma masomo hayo na faida baada ya kuhitimu "Ilani ya Uchaguzi inasisitiza kuwa na Elimu inayojikita katika Sayansi na Teknolojia kwa kuhakikisha Wanafunzi wanapata stadi na maarifa ya kujitegemea kulingana na Mazingira ya Nchi yetu. Aidha, Sera ya Nchi yetu ni kujenga Uchumi wa Viwanda ambao umejikita kwenye Sayansi na teknolojia" amefafanua Mkongo.
Kikao kazi hicho kimehitimishwa katika ukumbi wa Halmashauri hiyo huku kikiwa na maazimio ya kupandisha hali ya ufaulu, kukomesha utoro shuleni, ufuatiliaji wa ufundishaji, ushirikiano baina ya shule moja na nyingine .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza kwenye kikao cha tathimini ya matokea ya mtihani wa Taifa kuhitimu kidato cha nne na mtihani wa upimaji kidato cha pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Ndg.Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa kikao.
Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo, Mwl.Emmy Mfuru akizungumza wakati wa kikao.
Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe ametoa wito kwa walimu kuwa wazalendo katika uwajibikaji
Afisa taaluma idara ya sekondari Mwl.Abdnego Mulokozi akisoma taarifa ya hali ya ufaulu matokeo ya kidato cha nne.Kushoto ni Afisa taaluma Mwl.Neema Mbio.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wakati wa kikao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa