Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango atangaza neema kwa wananchi wa Meru, ambapo amesema Serikali itatoa magari matatu zikiwemo gari mbili za kubebea wagonjwa sambamba na kupanga watumishi wasiopungua 25 wa afya wakiwemo madaktari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Dkt Mpango amesema hayo baada ya kuzindua jengo la huduma za dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru, ampapo Serikali ilitoa Milioni 300 za ujenzi wa jengo hilo na milioni mia 509 za Vifaa tiba zikiwemo mashine za kisasa .
Aidha, Dkt.Mpango ametoa wito kwa watumishi wa afya hususani wa Kitengo cha huduma za dharura kuwahudumia wananchi kwa ufanisi, weledi na kujitoa kwani mgonjwa anapokuwa mahututi hupata faraja kwa namna anavyohudumiwa.
Vilevile Dkt. Mpango amewataka watumishi kulinda na kutunza miundombinu iliyopo kuleta tija zaidi ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira ya hospitali na kudhibiti ubadhirifu wa dawa ili wananchi waweze kunufaika na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi shupavu wa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Kuhusu changamoto kubwa ya Barabara katika Halmashauri hiyo Dkt.Mpango ameielekeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) kuona uwezekano wa kukarabati barabara za Halmashauri hiyo .
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda kwa niaba ya Wananchi wa Meru amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kutoa fedha nyingi za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru zikiwemo Bilioni 1.9 za uboreshaji sekta ya Elimu na Afya, Bilioni 1.6 za kurasimisha ardhi na Milioni 550 fedha za tozo kwa ajili ujenzi wa kituo cha afya Mareu na ukamilishaji wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule za Sekondari umoja Kingori na Muungano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa