Wananchi wa Kijiji cha Mareu, Kata ya King'ori Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameishukuru Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi Milioni 250 fedha za tozo za miamala ya simu kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kijiji hicho.
Wakizungumza Kwa nyakati tofauti Wananchi hao wameishukuru Serikali kutoa fedha hizo Milioni 250 kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya kwenye Kijiji Chao ambapo watapata huduma za afya katika umbali mdogo "tunamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha hizi kwani tulikuwa tunafuata huduma za afya Mkoa wa jirani au katika Hospitali ya Wilaya iliyopo mbali na kijiji hichi, hivyo niwaombe Watanzania wenzangu tushirikiane katika Kujiletea maendeleo" amesema Janeth
Naye Magdalena amesema Wanawake wa Kata ya King'ori hawana budi kumshukuru Mhe.Rais kwa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya kwani ni wanufaika wakuu hususani katika Swala la kujifungua "tunaishukuru Serikali kupitia fedha za tozo tutajifungulia Sehemu salama na kupata huduma Bora za afya.
Aidha, hayo yamejiri wakati Mhe.Dkt. Godwin Molel Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alipotembelea Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya akiambatana na Mhe.Dkt.John D Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ikiwa ni ziara ya Mhe.Mbunge kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo Jimboni sambamba na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Katika Ziara hiyo iliyowajumuisha Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.Jemsi Mchembe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili pamoja na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama na Wataalamu wa Halmashauri ya Meru Vituo vya Afya vilivyotembelewa ni Mareu, Makiba , Momela na Zahanati ya Songoro.
Maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo cha Afya Mareu ,ujenzi unaogharimu Shilingi Milioni 250 fedha za tozo za miamala ya simu.
Mhe.Dkt. Molel Naibu waziri wa afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dkt.John D.Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya na Mhe.Lukas Kaaya Diwani wa Kata ya King'ori wakati Wakizungumza na Wananchi wa Kijiji Cha Mareu.
Mhe.Dkt. Molel Naibu waziri wa afya maendeleo ya Jamii ,Jinsia,wazee na watoto alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Afya Mareu.
Mhe.Dkt. Molel Naibu waziri wa afya maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na watoto akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Makiba.
Mhe.Dkt.John D Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki akizungumza na Wananchi wa Kata ya Makiba
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili akizungumza na Wananchi wa Kata ya Makiba
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza wakati wa ziara ya Mhe.Munge Jimbo la Arumeru Mashariki katika Kata ya Makiba.
Ndg.Hungura Mbwana, Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa Ziara ya Mhe.Mbunge jimbo la Arumeru Mashariki, ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Miradi ya maendeleo .
Wananchi wa Kata ya Makiba wakati wa ziara ya Mhe.Mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki.
Mhe.Dkt. Molel Naibu waziri wa afya maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na watoto akikagua ujenzi wa Jengo la Kituo cha Afya Mareu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa