Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Wilayani Arumeru Ndg.Emmanuel Mkongo,akizungumza na mwandishi wetu, amesema Halmashauri hiyo inaendelea kuwachukulia hatua wamiliki wote wa vifaa vinavyo sababisha uharibifu wa mazingira kwa sauti(kelele) katika maeneo ya makazi na biashara.
Aidha Mkongo amesisitiza wamiliki hao kuzingatia viwango vilivyoainishwa kwa mujibu wa Kanuni ya udhibiti wa sauti na mitetemo ya mwaka 2015 ambayo imeelekeza kiwango cha sauti maeneo ya makazi kuwa decible 60 mchana na decibel 40 nyakati za usiku katika vipimo vya sauti(decible).
Akifafanua Viwango hivyo Afisa Mazingira kwenye Halmashauri hiyo Ndg.Charles Makama amesema lengo la kanuni hiyo ni kuhakikisha wananchi wakati wa mchana wanaendelea na shughuli zao sambamba na kuwasiliana bila usumbufu wa kelele na kwa vyakati za usiku wanapunzika bila usumbufu
Hivyo sauti ya Kiwango cha kipimo cha sauti 60 ni ile ambayo inakuwepo bila kuathiri mawasiliano umbali wa mtu na Mtu wazungumzapo huku kiwango cha decibel 40 ni kiwango cha sauti ile ambayo inaweza kuruhusu mtu kupuzika kwa kulala nyakati za usiku.
Pia, Afisa Mazingira huyo aliitaka jamii kuepuka uchafuzi huo wa mazingira wa kelele na mitetemo, ambao watu wengi wamekuwa wakidhani si tatizo badala yake waheshimu matakwa ya sheria na kanuni kwa nyakati za mchana na usiku. “ikidhibitishwa mtu amesababisha uchafuzi wa mazingira kwa sauti (kelele) atapaswa kulipa faini isiyopungua milioni 2 na isiyozidi Milioni 50,ama kifungo jela” amefafanua Makama.
Aidha Makama amesema kelele zinaweza sababisha ukiziwi,zinaathiri ukuaji wa ubongo haswa kwa watoto,zinaathiri nguvu za kiume kwani utulivu husaidia kupata nguvu za kiume za kutosha,Kelele huchangia kifo kwa watu wenye shinikizo la juu la damu.
Aidha Mkurugenzi Mkongo amehitimisha kwa kuwataka wananchi kuwaripoti wote wanaosababisha kelele katika ofisi za Serikali zilizo karibu nao au ofisi ya Afisa Mazingira wa Halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa