Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda ameongoza maandamano ya wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha katika upandaji miti na Usafi wa Mazingira katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Maandamano hayo yamefanyika ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa Kitaifa ambayo yamefanyika Tarehe 25 Julai, ambapo Mhe. Mkuu wa Wilaya alieleza kuwa Nchi ya Tanzania imerithi amani kutoka Kwa Mashujaa waliomwaga damu Kwa ajili ya kulinda amani .
" Amani tuliyonayo ni Tunu na amani hii tuliyonayo ni kama yai, yai likidondoka haliwezi kuunganishwa, amani hii tumeirithi Kwa wenzetu waliomwaga damu Kwa ajili ya Taifa letu. Ni jukumu letu sote kuilinda" Alisema Mhe. Kaganda.
Aidha, Mhe. Kaganda amewataka wananchi wote Kwa ujumla kuwaombea Mashujaa waliotangulia mbele za Haki ikiwa ni pamoja na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume Rais wa kwanza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Vilevile, amewataka wananchi katika kumbukumbu ya Mashujaa kuendelea kuwaombea Viongozi wote wa Serikali, Marais wastaafu na Marais waliotangulia mbele za haki, Kamati za Ulinzi na Usalama lakini kumuombea Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Utendaji wake Mungu ampe afya njema ili kuendelea kudumisha Amani Katika Nchi yetu ya Tanzania.
Pia, Alieleza kuwa Katika Maadhimisho ya kuwakumbuka Mashujaa wetu, Kila mmoja Kwa nafasi yake ahakikishe anaanzisha shughuli ya kishujaa kama utunzaji wa Mazingira kama alivyofanya Mama Thereza . Lakini kufanya matendo mengi ya kishujaa ambayo yanaacha alama nzuri Kwa jamii na Taifa kwa Ujumla.
Katika Maadhimisho hayo ameshiriki Mhe. Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki DKt. John D. Pallangyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Meru Mhe. Ndewirwa Mbise , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya pamoja na Viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa