Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg. Emmanuel J. Mkongo, kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 81 cha sheria ya Taifa ya uchaguzi Sura ya 343 rejeo la 2015 na kanuni ya 69(1)(d) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za Mwaka 2020, amemtangaza Dkt.John Danielson Pallangyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mshindi wa nafasi ya kiti cha Ubunge jimboni humo kwa kupata kura nyingi zaidi dhidi ya Bi. Rebecca Michael Mgondo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Tarehe 28 Octoba 2020.
Dkt.John D. Pallangyo amepata kura 84,858 na Bi.Rebecah Michael Mgondo amepata kura 14,688 ikiwa idadi ya wapiga kura walioandikishwa ni194,367 idadi ya waliopiga kura 100,885, kura halali 99,458 na kura zilizokataliwa ni 1427.
Aidha, Msimamizi huyo wa uchaguzi amemkabidhi Dkt.John D. Pallangyo cheti cha ushindi wa nafasi ya Kiti cha Ubunge.
Ikumbukwe kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa na wagombea toka vyama viwili tu CCM na CHADEMA.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg. Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi cheti cha ushindi wa nafasi ya kiti cha ubunge Dkt.John Danielson Pallangyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa