Chama cha Mapinduzi (CCM) cha ongoza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani Katika Jimbo la Arumeru Mashariki kwa wagombea wake kushinda nafasi za udiwani katika kata zote 5 zilizofanya uchaguzi kama ifuatavyo ,
Japhet J.Jackson wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) ameshinda nafasi ya Udiwani katika kata ya Ambureni kwa kupata kura 2057 na kumshinda mpinzani wake Dominick E.Mollel wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata 1201
Samson P. Laizer wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) ameshinda nafasi ya Udiwani wa Kata ya Makiba kwa kupata kura 2022 na kuwashinda wapinzani wake Joyce M. Lutha wa chama cha Demokracia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura 915 na Ernest G.Maturo wa ACT aliyepata kura 16
Yona N. Kaaya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameshinda nafasi ya Udiwani Kata ya Maroroni kwa kupata kura 3568 na kumshinda mpinzani wake wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Asenterabi L. Mbise aliyepata kura 1176
Anderson E. Sikawa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameshinda nafasi ya Udiwani wa Kata ya Leguruki kwa kupata kura 3023 na kumshinda mpinzani wake wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Rabiel F.Mbise aliyepata kura 287
Solomon L.Laizer wa Chama Cha Mapinduzi CCM ameshinda nafasi ya Udiwani wa Kata ya Ngabobo kwa kupata kura 820 na kumshinda mpinzani wake wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Emmanuel F. Salewa aliyepata kura 353
Aidha uchaguzi huu ulifanyika na kumalizika kwa amani na utulivu
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa