Tarehe 17 Septemba 2018 ,Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Meru umbali wa Kilometa 112.5 ili kukagua, kufungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi yenye thamani ya shillingi 14,931,815,390 katika Sekta za Maji, Elimu, Afya, Barabara, Kilimo, na uwekezaji.
Miradi hiyo yenye thamani ya Shillingi 14,931,815.390 ni kama ifuaatavyo.
#Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Irikolanumbe na barabara ya Ubungo Irikolanumbe uliopo Nkoarisambu/Ndoombo.
#Mradi wa afya Jengo la kinywa na meno Hospitali Wilaya ya meru (Tengeru) utazinduliwa.
#Mradi wa maji Kijij cha Nshupu utawekwa jiwe la msingi.
#Mradi wa Kilimo cha Vitunguu aina ya chives uliopo Kiwawa/Hortanzia utazinduliwa
#Mradi wa Kiwanda cha kuchakata kahawa-Tanzanate coffee uliopo UsaRiver-Kitongoji cha Magadirisho utazinduliwa.
#Shule ya Sekondari Fransalian iliyopo Kijiji cha Kitefu , kufungua madarasa, mabweni na maabara.
#Mradi wa Nyumba ya Watumishi wa Afya iliyopo Kijiji cha Malula.ambayo iliwekwa jiwe la msingi na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 utakaguliwa.
#Mradi wa Ghala la kuhifadhia nafaka lililopo Kata ya
King’ori Kijiji cha Muungano ambalo ni mradi lilifunguliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 utakaguliwa.
Aidha Mkesha wa Mwenge wa Uhuru utafanyika katika uwanja wa Shule ya Muungano -Usa -River
"Wote mnakaribishwa"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa