Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Timotheo Mnzava Amewataka vijana kuamka na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ili kupata maendeleo na kuwasisitiza kua na nidhamu kwenye matumizi ya Fedha,nidhamu ya kazi na nidhamu kwenye jamii jambo litakalo waletea maendeleo hayo.
Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutambua nafasi ya vijana kwenye Uongozi tofauti na hapo awali nakuwashauri vijana waliopata fursa mbalimbali zikiwemo za Uongozi kutumia nafasi hizo vizuri ili kuendelea kujenga imani kwa Serikali na Jamii kwa ujumla kua vijana wanaweza
Katibu Tawala huyo ameeleza hayo alipokua anafungua Mdahalo wa vijana Kwenye Halmashauri ya Meru uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo ukiwa na lengo la kuwajengea uwezo na kuwakumbusha vijana kutumia fursa zilizopo kwenye Halmashauri hiyo ,
Aidha mada mbalimbali za kuwawezesha vijana kupata elimu juu ya matumizi ya fursa kwenye kilimo,ufugaji,biashara,ujasiriamali na huduma za benki kama fursa, elimu juu ya madhara ya madawa ya kulevya ,namna ya kuacha kuyatumia,kuishi bila kutuma madawa ya kulevya na Ulinzi na usalama kijamiia matumizi sahihi ya mitandao ya na elimu juu y zilitolewa.
Naye afisa vijana Mkoa wa Arusha Japheth M. Kurwa amesema Ndani ya Mkoa huo kunafursa mbalimbali hivyo ni wakati wa vijana Kuchangamkia fursa hizo akisisitiza |"vijana muwe ni watu wa kutafuta fursa kwa kuulizia"
Katika matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ,Lubatuka Japhet ambaye ni mwenyekiti wa Tanzania leo amewataka vijana kutumia kijamii kama fursa nakunufaika na si vinginevyo
Walengwa ambao ni vijana wameishukuru Hamashauri ya Meru kwa kuandaa mjadala huu muhimu na kushauri kuwepo na utaratibu wa kukagua mkakati wa biashara kwa vijana wanaohitaji mkopo ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha za mikopo.
Aidha mgeni rasmi auliongoza kutumia fursa ya huduma ya afya iliyokua inatolewa bure kwa kupimaji maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) shinikizo la damu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa