Halmashauri ya Wilaya ya Meru yaongoza katika matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la Uwezo uliopima uwezo wa kusoma kingereza, Kiswahili na kufanya hesabu kwa majaribio ya kiwango cha darasa la pili kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 7hadi16.
Matokeo ya Utafiti huo ya mwaka 2017 yameonyesha Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeshika nafasi ya kwanza kati ya Wilaya 56 kwa watoto wa umri wa miaka 7 hadi 16 kujua kusoma Kiswahili, kingereza ba kufanya hesabu kwa asilimia 75.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi Mwl.Marcus Nazi amesema siri ya matokeo hayo maziri ni ufuatiliaji mzuri kuanzia ngazi ya Wilaya,Halmashauri , juhudi za walimu na ushirikiano mzuri toka kwa wazazi .
Mwl.Nazi ametoa Wito kwa wazazi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wamtoto kupata chakula cha mchana "Watoto wanapokuwa nyumbani wanakula chakula ,hivyo hivyo na wakiwa shuleni mzazi anawajibika kuhakikisha Mwanawe anapata vhakula cha mchana awapo shuleni"amesisitiza Mwl.Nazi
Mratibu wa shirika la Uwezo Kanda ya Kaskazini Bi. Asia Lembareti amesema utafiti huo unasaidia viongozi, wazazi na wadau wa elimu kupata ufahamu wa umahiri wa kweli kwa kila mtoto katika kusoma na kufanya hesabu hivyo kutafuta na kubaini changamoto na kuzitatua ili watoto kufanya vizuri kwenye masomo hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la CEDESOTA, Jackson E. Muro ambalo ni mdau wa Shirika la uwezo kwenye maswala ya elimu , ameipongeza Halmashauri ya Meru kufanya vizuri na kuitaka kuongeza juhudi ili kufanya vizuri kwa asilimia 25 iliyobakia ya watoto wa umri wa miaka 7 hadi 16 kusoma kwa umahiri Kingereza,Kiswahili na kufanya hesabu kwa kiwango cha maharibio ya darasa la pili.
Pia.Ametoa Wito kwa wazazi kutekeleza jukumu la watoto kupata chakula wanapokuwa shuleni pamoja na kuwasaidia watoto kujifunza kwa kuhakikisha watoto wanahudhuria shule,anafanya majaribio na kazi walizopewa shuleni nk.
Uzinduzi huo wa taarifa ya tathimini ya Shirika la Uwezo mwaka 2017 umefanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Amani na kujumuisha Maafisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Walimu wakuu ,maafisa elimu Kata ,Wanafunzi na Wawakilishi wa Wazazi.
Afisa Elimu Msingi Mwl.Marcus Nazi akizungumza wakati wa uzinduzi.
Mratibu wa shirika la uwezo Kanda ya Kaskazini Bi. Asia Lembareti akizungumza wakati wa uzinduzi.
Mkurugenzi wa Shirika la CEDESOTA, Jackson E. Muro.
Maafisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa uzinduzi.
Walimu wakuu ,maafisa elimu Kata wakati wa uzinduzi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Leganga na Usa-River.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa