Kuelekea miaka 59 ya Muungano Watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamejitokeza kufanya usafi katika maeneo mbali mbali ya Usa- River ikiwa ni utamaduni wa kutunza na kuifadhi mazingira.
Wakati wa zoezi hilo Katibu tawala wa Wilaya ya Arumeru Mwl. Jemsi Mchembe amesema moja ya tunu ambayo viongozi wametuachia ni kutunza mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ametoa wito kwa wananchi kujikita katika upandaji wa miti ili kukabiliana na ukame na uharibifu wa mazingira ambapo Halmashauri iliandaa miche ya miti elfu 32 na mpaka sasa imegawa miche elfu 20 kwa kata ya kikwe nq miche mingine imegawanywa kwa Kata za Marciano, Kikatoti,Nkoranga na Ngabobo pamoja na wananchi mmoja mmoja.
Viongozi wa Chama na wadau wa mazingira wametoa wito wa zoezi la usafi kuwa endelevu kwa kila mwananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao sambamba na kutunza vyanzo vya maji "Mazingira ni uhai kwetu hivyo hatuna budi kuyatunza "amehimiza Anankira Nanyaro ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kichama Meru
Diwani wa kata ya Usa River Mhe. Omari Mshana ametoa shukurani kwa viongozi wa Halmashauri, vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushiriki katika zoezi hilo la kufanya usafi na kuleta hamasa katika kata yake ambapo ameahidi zoezi hilo kuwa endelevu.
Mkurugenzi wa shirika la dunia la salama foundation Bw.Iddi Ningaametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na muamko na hamasa ya kuendelea kufanya usafi mara kwa mara.
0Tito Kitomari ambaye ni makamu mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani ametoa Wito kwa jamii kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwani hakuna mbadala wake.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa