Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameanza Zoezi la utengenezaji wa kamati za kulinda kuzuia na kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Mtoto Zoezi hilo limeanzia katika kijiji cha Nshupu likiongozwa na Martha Mzava Afisa maendeleo ya Jamii mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Mtoto.
Aidha katika uundaji wa kamati hiyo wanakamati wamepatiwa Mafunzo yatakayo wawezesha kupambana na matukio ya Ukatili kwa jamii inayowazunguka ambapo Moja ya watoa mafunzo ni Inspekta wa jeshi la Polisi Abeli mwakapalila amewataka kutohofu kutoa Taarifa pindi zinazopatikana kwani zitasaidia kupunguza vitendo hivyo vya kiualifu na kuwataka Wananchi kutoa ushirikiano Kwa jeshi la Polisi.
Aidha Diwani wa viti maalumu Kata ya Mbuguni Mheshimiwa Glory Kaaya amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto kwani wanawake wengi wamesahau swala zima la malezi nakujikita hasa kwenye utafutaji pia amewataka wanawake kutambua haki zao ili kuondokana na swala la kunyanyaswa katika Jamii
Mchakato wa uundaji wa kamati hizi za MTAKUWA unalengo wa kufikia vijiji 61 Kwa ifikapo mwezi wa 8
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa