Halmashauri ya Wilaya ya Meru, mapema hii leo, imekabidhi jumla ya vishikwambi 30 vilivyo tolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Maafisa Mifugo wa kata na vijiji . Zoezi hilo limefanyika katika Ofisi za Halmashauri.
Vishikwambi hivyo vitatumika kuingiza taarifa muhimu za mifugo katika Mfumo wa Taifa wa Utambuzi wa mifugo kwa wanyama wote watakao pata chanjo na kuwekewa hereni za kielektroniki kwa ajili ya Usajili, utambuzi na Ufuatiliaji wa Mifugo.
Akikabidhi vishikwambi hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Dkt. Charles Msigwa ambaye ni Mratibu wa zoezi hilo, aliwataka maafisa kuhakikisha wanavitumia kwa ufanisi ili kusaidia kuboresha mifumo ya taarifa katika sekta ya mifugo. Alisisitiza kuwa teknolojia hiyo ni nyenzo muhimu katika mageuzi ya sekta ya mifugo, hususan katika kipindi hiki ambacho serikali inalenga kuongeza mchango wa mifugo katika uchumi wa taifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa