Waheshimiwa Madiwani wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameridhia na kupitisha Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru Kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 yenye jumla ya Shilingi za Kitanzania Bilioni Sitini na Nne, Milioni Mia Saba Sabini na Tatu, Laki Nne Sabini na Sita, Mia Tatu Kumi na Nne na Senti Sitini na Moja. ( Tsh. 64,773,476,314.61).
Akiwasilisha Muhtasari wa Bajeti hiyo, katika Mkutano Maalum wa wa kujadili rasimu ya mpango na bajeti uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri leo tarehe 07 Februari 2025, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo , Mhe. Jeremia Kishili ametoa mchanganuo wa bajeti hiyo kama ifuatavyo:-
- Mapato ya Ndani Tshs. 6,308,122,658.61
- Ruzuku ya Mshahara Tshs. 45,815,301,800.00
- Ruzuku ya Matumizi Mengineyo Tshs. 2,366,164,000.00
- Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo Tshs. 10,283,890.00
Aidha, Mhe. Kishiri ametoa shukrani kwa Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi inayoendelea kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuifanya Halmashauri ya Meru kuendelea kuletewa fedha za kutekeleza miradi mingine.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa