Halmashauri ya wilaya ya Meru imefanikiwa kutoa mafunzo ya Ujasiriamali Kwa Vikundi vyawanawake mbalimbali.
Kikundi cha wanawake wajasiriamali NEW HOPE GROUP kutoka Kata ya Nkoaranga Halmashauri ya Wilaya Meru kimepata mafunzo ya vitendo ya ujasiriamali kuhusu utengenezaji wa vitambaa vya batiki na sabuni za majumbani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kuwajengea uwezo wa kujiajiri.
Mafunzo hayo yamefanyika katika mtaa wa jua kali Kata ya Nkoaranga Wilaya ya Arumeru yakiratibiwa na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikiana na shirika la,Women Empowerment Circle (WEC)
Baadhi ya wanawake kutoka Kata hiyo wameweza kujitokeza kujishughulisha na Mafunzo hayo ikiwa ni sehemu yakuongeza ujuzi na maarifa katika swala zima la ujasiriamali
Washiriki waliweza kujifunza hatua Kwa hatua namna ya kuchanganya rangi za batiki kuchora na kukausha vitambaa pamoja na mbinu Bora za kutengeneza sabuni za maji na za mche kutoka shirika la Viwanda vidogo (SIDO) yakitolewa na mwalimu Zulfa Said.kikundi hicho kiliweza pia kupatiwa Mafunzo ya namna ya kupakia ,kupangilia bidha,kupanga bei za bidhaa na kuuza katika soko la ndani nala nnje.
Hata hivyo Kwa mujibu wa Mratibu wa mafunzo hayo kutoka halmashauri ya Meru ofisi ya maendeleo ya jamii Paulina Matinde amesema lengo kuu ni kuwawezesha wanawake kuanzisha miradi ya uzalishaji inayohitaji mtaji mdogo lakini yenye faida kubwa.Aliongeza Kwa kusema batiki na sabuni ni bidhaa zinazotumika kila siku. Tunataka wanawake waone kuwa wanaweza kuzalisha bidhaa hizo kwa ubora unaokidhi soko, hata nyumbani kwao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa