Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wiaya ya Meru Mwl.Sara Kibwana amesema Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla ngazi ya Mkoa kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yaliyofanyika tarehe 06 Juni 2018 hadi 10 Juni 2018 ambapo Halmashauri 7 za Mkoa wa Arusha zilishiriki .
Mwl.Kibwana amefafanua kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imezawadiwa vikombe 5 kutokana na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu wavulana, Mpira wa wavu wasichana, Mpira wa mikono wasichana na Mpira wa kengele pia ilikuwa mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa wavu wavulana.
Mwl.Kibwana amesema siri ya ushindi huo ni pamoja na maandalizi mazuri yaliyofanyika kwani Halmashauri hiyo ilitoa maelekezo zaidi ya miezi 9 iliyopita kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuhakikisha kila wiki wanafunzi wanakua nasiku za kufanya michezo pia maandalizi yalikuwa mazuri wakati wa michezo kwakuwa wachezaji walijiandaa kikamilifu kwa kukaa siku 5 kambini.
Naye Afisa utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Senyaeli Pallangyo amesema uchaguzi wa wachezaji kwa kuzingatia viwango uliofanyika kuanzia ngazi ya chini hadi Wilaya umechangia ushindi huo mkubwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa makocha sambamba na wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kufuata taratibu za michezo .
Jumla ya wachezaji 25 kutoka timu mbalimbali za Halmashauri yaWilaya ya Meru na Makocha 4 wamechaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Arusha .
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka huu 2018 imekuwa mshindi wa kwanza na wajumla kwa ngazi ya Mkoa wa Arusha wenye Halmashauri 7 katika mashindano ya michezo ya umoja wa michezo Shule za Sekondari Tanzania ( UMISSETA) na umoja wa michezo na taaluma shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na kuzawadiwa jumla ya Makombe ya ushindi 10
vikombe 5 vya ushindi wa Mashindano ya UMITASHUMTA kuwa mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu wavulana, Mpira wa wavu wasichana, Mpira wa mikono wasichana na Mpira wa kengele pia ilikuwa mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa wavu wavulana.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru ,wakuu wa Idara/Vitengo pamoja na watumishi wengine wakati wa mapokezi ya vikombe 5 vya ushindi katika ,mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu wavulana, Mpira wa wavu wasichana, Mpira wa mikono wasichana na Mpira wa kengele pia ilikuwa mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa wavu wavulana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa