Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akiwa na kikombe cha ushindi mara baada ya halmashauri hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kati ya halmashauri zote za Kanda ya Kaskazini kwa kuwa na banda lenye mifugo bora zaidi wakati wa ufungaji Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini Eneo la Themi Njiro Jijini Arusha.
Aidha, banda la Halmashauri ya Wilaya ya Meru limekuwa kivutio kikubwa kwa kuwa na aina mbalimbali ya mifugo bora na yenye tija kwa mfugaji ambapo wataalam waliobobea kwenye kilimo wametumia maonesho hayo kutoa elimu ya teknolojia za ufugaji wanyama zikilenga
Ufugaji wenye tija pamoja na mnyororo wa thamani kufikia Ajenda 10- 30 Kilimo Biashara.
Mwl.Zainabu amebainisha kuwa, Serikali imeendelea kuwezesha wakulima na Wafugaji kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo ili kufikia Ajenda 10-30 ya Kilimo Biashara.
Kauli Mbiu ya Nanenane 2022 ni "AJENDA YA 10 -30 KILIMO NI BIASHARA 'SHIRIKI KUHESABIWA KWA MIPANGO BORA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI"
Karibuni Meru tunamifugo bora na tunaongoza kwa kilimo cha mbogamboga mkoa wa Arusha.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa