Ikiwa ni maadhimisho ya kilele cha siku ya Vijana duniani tarehe 12 Agosti 2022, Wilaya ya Arumeru imepiga marufuku makampuni na watu binafsi wanaotumia kigezo cha fursa kuwatapeli na kuwakandamiza vijana kuacha mara moja.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, mwakilishi wa Mkuu wa ya Arumeru Mwl.Marcus Nazi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi wa halmashauri hiyo ametoa wito kwa vijana kuitumia vema fursa mbalimbali kujikwamua kiuchumi ikiwemo fursa ya mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri .
Mwl.Nazi amesema serikali imeweka mikakati kupitia sera mbalimbali za kuwaletea vijana maendeleo kwa kuzingatia kundi la vijana ni kundi kubwa kwani tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 65% ya wa Waishio bara la *Africa*= *Afrika* ni vijana ambapo ametoa wito kwa wadau kuungana na serikali kuwasaidia vijana na si kuwakwamisha kwani Serikali wilayani humo haitosita kuwachukulia hatua Makampuni au watu binafsi wanaowakandamiza vijana kwa kigezo cha fursa .
Elisante Nnko ambaye ni miongoni mwa vijana walioshiriki maadhimisho hayo ametoa wito kwa vijana imani waliojengewa kwenye jamii na serikali kwa kuchapa kazi kwa weledi na bidii.
Maadhimisho hayo ya siku ya vijana yaliyofanyika katika viwanja vya MS TCDC yamewezeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika ya SOS CHILIDREN'S VILLAGES, VOICE OF YOUTH TANZANIA, DUSAFO, SAVE AFRICA TANZANIA ,TAMIHA,KAMBELE
Ikumbukwe Kila tarehe 12 ya mwezi Agosti Dunia huadhimisha siku ya Vijana,ikiwa lengo ni kukumbuka mchango wa vijana katika kukuza maendeleo na kaulimbiu ya mwaka huu ni "Kuelekea 2030: Tanzania ya viwanda,BORESHA ELIMU Kwa vijana,kwa maendeleo ya Taifa".
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa