Halmashauri ya Meru yaanza utekelezaji wa mfumo jumuishi wa usimamizi wa mashauri ya Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo imetoa mafunzo kwa wasimamizi wa mashauri ngazi ya jamii (CCW), watendaji wa vijiji, maafisa ustawi wa jamii na maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya Kata,
Akifungua mafunzo hayo kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Charles Makama ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mazingira ametaka washiriki kutumia mafunzo hayo kikamilifu ili kuwatambua na kuwapa huduma watoto wote wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Aidha, Makama amesema utekelezaji wa mfumo unaotekelezwa na serikali Kwa kushirikiana mradi wa KIZAZI hodari unaotekelezwa na ELCT ulianza mwaka 2017 katika halmashauri 81 zikiwemo halmashuru za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambapo umetekelezwa kwa miaka 5 na kwa sasa ni fursa kwa Halmashauri ya Meru ambapo Mfumo huo unalenga kuwafikia watoto elfu saba wa mkoa wa Arusha wakiwemo watoto wa Meru.
Afisa ustawi wa jamii Mkoa Ndugu Denis Mgiye ambaye pia ni mwezeshaji kwenye mafunzo hayo ametoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha watoto wanahudumiwa ikiwa ni pamoja na kuwaibua watoto wenye changamoto ili waweze kuunganishwa na huduma muhimu kama lishe, afya, elimu n.k na kuhakikisha tunakuwa na kizazi ambacho ni salama "nitoe wito kwa jamii kuwalinda na kuwasaidia watoto waishio kwenye mazingira hatarishi kwani mtoto ni wajamii"amehimiza Mgiye
Mafunzo hayo yanaendelea kwa siku kuanzia tarehe 13 hadi 18 Septemba 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mshikanano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa