Kuelekea siku ya vijana Duniani tarehe 12 Agosti 2022 vijana toka Hamashauri ya Wilaya ya Meru wameshiriki shughuli za kijamii kwa kufanya usafi katika kituo cha afya Usa -River pamoja na kuwafariji wagonjwa .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana hao wamesema wanajivunia kuwa vijana na watatumia umri wao kuisaidia jamii na nchi kwa kufanya kazi kwa bidii "sisi ni vijana wa leo na wazee wa kesho hatuna budi kuutumia ujana wetu kuisaidia jamii inayotuzunguka na nchi yetu kwa ujumla"Amesema Michael Nnko miongoni mwa vijana waliojitokeza kushitiki usafi
Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Halmashauri hiyo Bi.Regina Tilya ametoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele kushiriki shughuli za kijamii na za maendeleo ambapo pia amewakumbusha wazazi kuwa vijana bado wanahitaji malezi na ushauri ili kuwa na jamii bora yenye maadili na ustawi mzuri.
Vilevile Vijana hao kwa kwa kushirikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya SOS CHILIDREN'S VILLAGES, VOICE OF YOUTH TANZANIA, DUSAFO, SAVE AFRICA TANZANIA ,TAMIHA, KAMBELE wametoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho cha afya ili kutoa motisha kwa vijana kuendelea kuwa msaada ndani ya jamii.
Mmoja wa wadau wa mashirika hayo Bw. Philipo Namanga Afisa vijana kutoka shirika la SOS Childeren's Villages Arusha amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kushiriki shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na wakuwatembelea watu wenye uhitaji maalumu nakuwapatia msaada pale wanapohitaji.
Akizungumza kwa niaba ya Daktari wa kituo cha afya Usa River Pascal Urio ambaye ni mtaalum wa dawa za usingizi Amewashukuru vijana na mashirika hayo kwa kuweza kufanya usafi katika hospitali hiyo pamoja na kutoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa.
Maadhimisho ya siku ya vijana katika halmashauri ya Wilaya ya Meru yatafanyika tarehe 12 Agost 2022 katika ukumbi wa MS TCDC.
KILA MMOJA ANAHUSIKA KATIKA KUJENGA UCHUMI IMARA ,USTAWI NA MAENDELEO ENDELEVU ,JIANDAE KUHESABIWA
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa