Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameagiza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Patandi kukamilika kwa wakati na kwa ubora.
Makwinya ametoa agizo hilo wakati akizungumza na kamati za ujenzi wa Mradi huo, Walimu, Viongozi ngazi ya Kata na Vijiji pamoja na fundi, na kuwahimiza kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kuharakisha kasi ya ujenzi "Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan anawathamini watoto wenye mahitaji maalum ambapo ametoa fedha hizi Shilingi milioni 80 kuwajengea bweni, hivyo hamna budi kushirikiana na kusimamia ujenzi huu ukamilike kwa wakati na kwa viwango "amehimiza Makwinya
Vilevile Mwl.Makwinya amemtaka fundi wa Mradi huo Ndg.Kanankira Somi kuongeza idadi ya vibarua pamoja na mafundi ili kurahisisha ukamilishaji wa Mradi "fundi ukiongeza idadi ya vibarua hauongezi gharama bali unapunguza siku za kufanya Kazi kwani kazi ambayo ingefanywa na vibarua 5 kwa Siku 10 itafanywa kwa Siku 5 na vibarua 10 "amefafanua Makwinya
Pia.Makwinya amewaagiza wataalam akiwemo Mhandisi wa ujenzi, Afisa manunuzi na Mkuu wa Shule hiyo kuhakikisha wanafuatilia ujenzi huo kwa karibu, kukagua na kushauri kwa kila hatua ya ujenzi "Mhandisi wa ujenzi hakikisha fundi anafika eneo mradi kwa wakati na kazi zinafanyika na Afisa manunuzi hakikisha vifaa vinapatikana kwa wakati
" Ameelekeza Makwinya
Naye Mhe.Julius Mungure Diwani wa Kata ya Akheri, unapotekelezwa Mradi huo bweni hilo ameishukuru serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutambua umuhimu wa kuwajengea fursa na mazingira mazuri ya kusoma watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa Milioni 80 kwaajili ya ujenzi wa bweni.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Patandi Jackline Mtui amesema ujenzi wa bweni hilo utasaidia usalama kwa watoto sambamba na watoto hao kuhudhuria mafunzo kwani wengi wanaishi mbali na Shule na mara nyingi hushindwa kuhudhuria masomo kutokana na gharama za usafiri .
Aidha,Serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha za Kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Milioni 250 fedha za tozo kujenga Kituo cha Afya Mareu ,Milioni 300 fedha za UVIKO -19 kujenga Jengo la dharura katika Hospitali ya Wilaya, Milioni 470 kujenga Shule mpya ya Sekondari Ambureni ,
Milioni 80 kujenga bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Patandi.
Pia. Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwa robo ya kwanza ya mwaka 2021/2022 imetoa Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Maroroni.
Ikumbukwe
Serikali ilitoa Bilioni 1.4 za ujenzi wa Vyumba 70 vya Madarasa katika shule za Sekondari ambapo tarehe 29 Desemba 2021 Madarasa hayo yalikamilika.
*Kazi iendelee*
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa