Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikiwa ni Siku ya miaka 60 ya uhuru kwa Kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa Bonanza la kuhamasisha chanjo ya Uviko-19 ambapo kumekuwa na michezo ya Mpira wa miguu na kukimbiza kuku sambamba na maonyesho mbalimbali
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ametoa wito kwa jamii kuchukua tahadhari ya Uviko-19 kwa kupata Chanjo "nipongeze timu zote zilizoshiriki Mpira wa miguu na mbio za kukimbiza kuku ,ikiwa Leo ni siku ya Miaka 60 ya uhuru niwasihi tuishi ndani ya kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku hii ambayo MIAKA 60 YA UHURU TANZANIA IMARA, "amehimiza Makwinya
Mwl .Makwinya amesema mafanikio ya miaka 60 ya uhuru katika Halmashauri hiyo ni pamoja na uwepo wa Hospitali mbili, Vituo vya afya Kumi ,Zahanati 32 ,Shule za Sekondari 66 (za serika 37 zisizo za Serikali 29), Shule za Msingi 173 (za Serikali 116 na zisizo za Serikali 57).
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus amesema kwa sasa chanjo za UVIKO-19 inapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ambapo ametoa wito kwa jamii kuchukua tahadhari ya Uviko-19 kwa kupata Chanjo .
Diwani wa Kata ya kikwe Mhe.Daniel Kaaya ameishukuru Serikali kwa kuleta chanjo hiyo ya UVIKO-19 ,ambapo amewasihi Wananchi kuchukua tahadhari kwa kupata Chanjo
Aidha Timu ya Meru Veteran Imeibuka mshindi kwa kuifunga timu ya watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya jamii Tengeru kwa bao moja katika bonanza hilo la kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari ya Uviko-19 kwa kupata Chanjo katika Uwanja wa Ngarasero Usa-River ambapo kwa upande wa mbio za kukimbiza kuku Renatus Magembe toka timu ya Walimu ameibuka mshindi.
Afisa michezo Halmashauri Daniel Nanyaro amesema jamii haina budi Kushiriki Michezo mbalimbali kwaajili ya kuimarisha afya "Michezo ni afya na huimarisha mahusiano kwani huleta umoja katika maeneo ya kazi na jamii kwa ujumla "amesema Nanyaro Baadhi ya picha za tukio.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akikabidhiwa kikombe Cha ushindi kwa timu ya Meru VETERANS
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa