HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
Tukielekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto WA Africa ambayo huadhimishwa kila Mwaka Juni 16 Leo Juni 15 Halmashauri ya Wilaya ya Meru imefanya Maadhimisho hayo yaliyo fanyika katika Shule ya Msingi Silver Leaf, Maadhimisho yaliyohudhuriwa na watoto kutoka shule mbali mbali, Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali
Maadhimisho yaliyokwenda na kauli mbiu isemayo " ELIMU JUMUISHI KWA WATOTO: IZINGATIE MAARIFA, MAADILI NA STADI ZA KAZI" Kauli mbiu hiyo ikiwa na Lengo kubwa lakumuandaa Mtoto kuweza kukabiliana na Mazingira yanayo Mzunguka.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo Ni Erena Materu Afisa maendeleo ya jamii Dawati la Maendeleo ya Mtoto Mkoa wa Arusha ambaye amewataka wazazi, walezi na walimu kuwapatia watoto stadi mbali mbali za maisha na kuwajengea uwezo wakutumia vipaji vyao ili viweze kuwasaidia katika Mazingira yakila siku.
Materu ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwakuendelea kushirikiana na Taasisi mbali mbali ili kuweza kuwasaidia watoto wanaohitaji msaada.
Miongoni mwa hayo Materu ameaihidi kutoa ushirikiano Pindi anapohitajika na kuahidi kushirikiana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwenda Kutatua kero zilizowasilishwa na watoto hao kupitia Risala.
Sambamba na hayo Mgeni Rasmi amekabithi vyeti vya kuthamini mchango wa wadau mbali mbali walioweza kujitoa ili kufanikisha zoezi la kuwakusanya watoto Kwa pamoja Kwa lengo la kupatiwa elimu na kuburudika kwa pamoja.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa