Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Mkoani Arusha imefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita kwa kushika nafasi ya pili kitaifa kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo, huku shule ya Sekondari Kibaha ikishika nafasi ya kwanza na shule ya Sekondari Kemebos ikishika nafasi ya tatu,hii ni kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na baraza la mitihani Taifa.
Aidha matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri ni mwendelezo wa historia ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita kwani kwa miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa ,ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza,mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa kwa watahiniwa wake 67 kupata daraja la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata daraja la pili.
Nuru ya shule hii ya Sekondari Kisimiri yazidi kuangaza kwenye Mkoa wa Arusha wenye shule 31 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na Binafsi kwani ni shule pekee ya Serikali kushika nafasi ya kwanza mkoani hapa kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher Kazeri alipokuwa akiwapongeza walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa jitihada zao zilizo ifanya shule hiyo kuwa mshindi wa pili kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2018, pia amewasihi walimu hao kuongeza bidii katika ufundishaji ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa.
Mkurugenzi huyo ametoa pongezi hizo alipotembelea Shule hiyo kwa Lengo la Kuwapongeza Walimu pamoja na kusikiliza na kutatuo changamoto wanazokabiliana nazo ili kuleta tija zaidi kwenye taaluma ya Shule hiyo.
Makamu mkuu wa shule ya Sekondari Kisimiri Mwl. John Awe amesema kuwa mojawapo ya mbinu zilizotumika kuhakikisha shule hiyo inapata matokeo mazuri illikuwa kutoa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi ambao walikuwa na uwezo mdogo, hivyo walimu walitenga muda wa ziada kuwafundisha wanafunzi hao ambao wengi wao walifanya vibaya kwenye mtihani wa utamirifu (MOCK) kwa kupata alama sifuri.Ameongeza pia walimu wana moyo wa kufundisha kwa kutoa mfano kuwa kwenda darasani ni swala moja na kufundisha kama inavyotakiwa na wanafunzi kuelewa ni jambo jingine .
Nao Walimu wametoa changamoto zinazoikabili Shule hiyo ni upungufu wa viti vya walimu 50 pamoja na madawati ya wanafunzi 300 pia walimu hao wamehitaji ufafanuzi wa maslai yao kama watumishi ikiwemo kupanda daraja,
Akitoa ufafanuzi wa maswala ya watumishi Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu .Grace Mbilinyi ameeleza kuwa kutokana na zoezi la kuwabaini watumishi hewa na wenye vyeti vya kugushi Serikali ilisitasha upandaji madara kwa watumishi wa umma ila kwa sasa maelekezo mbalimbali yanatolewa ambapo zoezi hilo linaendelea kwa awamu pia
Kuhusu swala la malipo ya likizo amewasihi walimu kuwa makini kwa kuweka viambatanisho vyote muhimu vikiwemo vyeti vya watoto vya kuzaliwa na vyeti vya ndoa pia ametoa angalizo la udanganyifu kwa kugushi vyeti hivyo.
BAADHI YA PICHA YA TUKIO LA KIKAO CHA PONGEZI .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher Kazeri alipofika kwenye Shule ya Sekondari Kisimiri na kupokelewa na Makamu mkuu wa shule ya Sekondari Kisimiri Mwl. John Awe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher Kazeri akitoa pongezi kwa walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa jitihada zao walimu zilizo ifanya shule hiyo kuwa mshindi wa pili kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher Kazeri akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri.
Nyuso zinazoashiria kufurahia ushindi wa Shule ya Sekondari Kisimiri kushika nafasi ya pili kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha Sita mwaka 2018,Kulia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher Kazeri ni Makamu mkuu wa shule ya Sekondari Kisimiri Mwl. John Awe
Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu ,Grace Mbilinyi Akitoa ufafanuzi wa maswala ya watumishi yaliyoulizwa na walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri.
mwakilishi wa Afisa elimu Sekondari Mwl. Angela Urasa alipokuwa akiwapongeza walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri
Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri walipo kuwa kwenye kikao cha pongezi baina yao na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri walipo kuwa kwenye kikao cha pongezi baina yao na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri walipo kuwa kwenye kikao cha pongezi baina yao na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri walipo kuwa kwenye kikao cha pongezi baina yao na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Picha ya pamoja ya viongozi toka wa Halmashauri na walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa