Uwekaji saini Mkataba wa ukandarasi kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Mshele Investment umefanyika leo katika ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya mchakato wa Zabuni ya ukandarasi wa ujenzi wa nyumba 3 za Wakuu wa Idara kukamilika kupitia mfumo wa Nest ambapo gharama ya mkataba ni kiasi cha Tsh 300,000,000.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jeremia Kishili amesisitiza ujenzi ufanyike kwa ubora na viwango vinavyotakiwa lakini pia, kuzingatiwe muda wa utekelezaji wa mradi kulingana na makubaliano ya mkataba.
Hata hivyo, amewataka wasimamizi wote wa mradi kuzingatia vigezo na masharti ya mkataba ili kusitoke migogoro na tofauti yeyote wakati wa utekelezaji wa Mradi.
Aidha, ameshauri mkandarasi aunge juhudi za Halmashauri kwa kununua tofali zinazotegenezwa na Halmashauri kwa kuwa na ubora stahiki. Mradi huu utaleta tija na kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara kwani watakuwa karibu zaidi na mazingira ya kufanyia kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa