Wito watolewa kwa walimu wa shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Wilayani Arumeru kuweza kuzingatia mafunzo kufundisha stadi za Kusoma,Kuandika na Kuhesabu ( KKK) yaliyoendeshwa katika Klasta tano za Halmashauri hiyo.
Wito huo umetolewa na
Afisa elimu Msingi wa Halmashauri hiyo Mwl.Marcuz Nazi ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo , wakati wa ufunguzi mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa walimu Wakuu wa shule za msingi , walimu wa taaluma , Maafisa Elimu Kata katika clasta ya Leganga ,na katika ukumbi wa shule ya msingi ya Amani.
Mwl Nazi amesema kutokana na tathmini iliyofanywa na idara ya yake kuonesha kuwepo kwa ongezeko la wanafunzi wasiomudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, Sambamba na uwepo wa changamoto ya ufundishaji katika madarasa ya Awali,darasa la Kwanza na darasa la pili ni sababu zilizosukuma uwepo wa mafunzo hayo.
Pia.Mwl.Nazi amesema mafunzo hayo ni mkakati wa Halmashauri hiyo kuwajengea walimu wote uwezo wa kufundisha kwa umahiri stadi za KKK ili kuondoa asilimia 12% ya wanafunzi wote wa shule za msingi za Halmashauri hiyo wasiomudu stadi za KKK, "Ilizoeleka madarasa ya awali,la kwanza na la Pili kufundishwa na walimu wenye umri mkubwa ambao wengi wao sasa wanastaafu, baadhi wamehama hivyo kusababisha uwepo wa changamoto ya ufundishaji wa madarasa hayo.
Nazi ameto wito kwa walimu wakuu wa Shule za msingi ,walimu wa taaluma na Maafisa Elimu Kata waliohudhuria mafunzo katika vituo 5, kuyasimamia mafunzo hayo na kuhakikisha walimu wanapata umahiri wa kufundisha stadi hizo za KKK "tumewapa mafunzo nyie viongozi ili mjue mnasimamia nini, na kama wawezeshaji wa walimu hivyo mtakapo rudi Mashuleni hamna budi kuwawezesha walimu kufundisha kwa umahiri KKK.
Nazi amewataka walimu kuondakana na dhana ya umri katika kufundisha " " Zama hizi ni Walimu wote kumudu kufundisha KKK kwa umahiri " amesisitiza Mwl. nazi.
Afisa Taalumu Msingi Mwl.Enock Sangova amesema mbali na jitihada za Halmshauri hiyo katika kuongeza hali ya ufaulu kwa madarasa ya mtihani, ambapo katika mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2020 asilimia ya ufaulu imeongezeka kutoka .92.5 hadi 93.2, hivyo uwepo wa wanafunzi wasiomudu stafi za KKK ni changamoto katika ufaulu.
Mwl.Sangova amefafanua kuwa mafunzo hayo yataleta mafanikio katika swala la taaluma kwani yamelenga mambo makuu mawili ambayo ni Kuondoa kabisa wanafunzi wasiomudu stadi za KKK katika Halmashauri ya Meru ifikapo June 2021 ambapo watafanya tathmini ya hali ya utejelezaji na kupima wamefanikiwa kiasi gani.
Pia. Kuondoa changamoto ya baadhi ya walimu kutokuwa na uwezo wa kufundisha madarasa ya Awali,lakwanza na lapili na kwamba baada ya mafunzo changamoto hiyo haitakuwepo tena.
Aidha, Sangova ameeleza mpango wa Idara ya Elimu Msingi ni kufanya mwendelezo wa mafunzo hayo kwa kuyafanya mara moja kwa kila muhula jambo litakaloboresha sana taaluma ya Halmashauri yetu ya Meru.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kwani walikua wakifundisha bila kuzingati hatua za kufundisha KKK.
Mwl. Aimbora Nnko ambaye ni Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makumira amesema Mafunzo hayo ni fursa ya kuongeza walimu wa kufundisha KKK kwani kwa kushirikia na Mwlimu wa taaluma pamoja na Afisa elimu Kata watawajengea uwezo Walimu wengine wa kufundisha kwa umahiri KKK.
Miongoni mwa Maafisa elimu Kata Mwl.Betram Sarapahi ameishukuru Halmashauri hiyo kwa kutoa mafunzo kwani itawasaidia wao kama Viongozi kusimamia jambo wanalolifahamu.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili kwa kujumuisha walimu wakuu 115 toka Shule 115 za umma, walimu wataaluma 115, waratibu 26 na walimu wawezeshaji 16.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Meru ina jumla ya shule 171 ,shule za Serikali ni 115. na Shule za binafsi ni 56 .
Afisa elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwl.Marcuz Nazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya stadi za KKK.
Mwenyekiti wa Maafisa elimu Kata Mwl.Godson Ndosi akizungumza wakati wa mafunzo ya stadi za KKK, kulia ni Afisa taaluma Msingi Mwl.Enock Sangova.
Mwl.Aimbora Nnko, Mkuu wa Shule ya Msingi Makumira akitoa maonii juu ya nafunzo ya stadi za KKK.
Walimu wakuu wa Shule na Walimu wa taaluma za Msingi wakati wa mafunzo ya stadi za KKK.
Wawezeshaji wa mafunzo ya stadi za KKK.
Maafisa Elimu Kata wakati wa mafunzo ya stadi za KKK.
Walimu wakati wa mafunzo ya KKK.
Mwl.Betram Sarapahi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa