Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itatatua changamoto zote za wananchi hivyo wasiwe na wasiwasi.
Mhe.Rais Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kikatiti, Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru.
Ambapo, amesema Changamoto zote ikiwa ni Barabara, Maji na kituo cha Afya Kikatiti zote zitafanyiwa kazi.
Katika kuendeleza Zahanati ya Kata ya Kikatiti Mhe. Rais Samia Saluhu ametoa shilingi Milioni 10 zakusaidia kuboresha Zahanati hiyo ili kiweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akiwa Wilayani Arumeru, Mhe.Rais Amesimama na kuwasalimu Wananchi katika maeneo ya Kikatiti, Usa-River na Tengeru.
Aidha, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amewasili Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo atatembelea mradi wa Maji wa Chekereni, atazindua hospitali ya Wilaya Jiji la Arusha na kuzungumza na wananchi katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid. Kisha atazindua kiwanda cha Nyama Longido, uzinduzi wa mradi wa Maji Longido na atafanya Mkutano wa hadhara stendi mpya Longido.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa