Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru washauriwa kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ambukiza,hayo yamesemwa na Ndg.Edward Chitete alipozungumza kwa niaaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru baada ya Watumishi wa makao makuu na Idara ya Afya wa Halmashauri hiyo kufanya mazoezi ya viungo kwa zaidi ya masaa 2 ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya akili.
Ndg.Chitete amewakumbusha wananchi siku ya kufanya mazoezi Kitaifa ni kila siku ya jumamosi ya juma la pili la mwezi ambapo Serikali iliona ni vyema kuwa na siku maalumu ili wananchi na watumishi wake kuimarisha miili yao na kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza baada ya mazoezi hayo Daktari Charles Migunga ambaye ni mratibu wa afya ya akili kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema mazoezi huimarisha miili na huepusha magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya akili mtu anapofanya mazoezi anapunguza msongo wa mawazo hivyo kuepuka ugonjwa wa akili uitwao SONONA (Dipression) pia hofu na woga uliopitiliza mara nyingi huwapata watu wasiofanya mazoezi.
Naye afisa michezo wa Halmashauri hiyo Aimbora Nnko amesema ipo mikakati mbalimbali iliyoandaliwa kuhakikisha Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wanatambua umuhimu wa mazoezi ya viungo pamoja na michezo na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi pia ameeleza katika kuhakikisha Meru inasikika kwenye ulimwengu wa michezo.
Ndg.Aimbora amefafanua kuwa ofisi yake imejipanga kuhakikisha vijana wanatumia michezo kama fursa kwa kuandaa mabonanza kwa vijana wa umri tofauti yenye lengo la kuibua vipaji pamoja na kuunda timu za michezo mbalimbali na kuimarisha zilizopo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa