Muonekano wa sasa wa kituo cha Afya Usa - River ni matumaini ya utatuzi wa upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa Kata ya Usa- river,muonekano huu unatokana na ujenzi wa miundombunu mbalimbali ulioanza mwezi Februari.
Aidha Serikali katika kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya kwenye umbali mdogo ilitoa fedha kiasi cha Tsh.milioni 500 kwa vituo vya afya 200 kwaajili ya uborehaji wa miundombinu.
picha zifuatazo zinaonesha baadhi ya matumizi ya milioni 500 iliyotolewa kwa kituo cha Afya Usa-river .
Picha ya jengo la upasuaji pindi litakapoanza kutumika kwa kiasi kikubwa litapunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya.
Jengo la wodi ya Mama na Mtoto ,pindi litakapo kamilika kinamama zaidi ya 40 watakaojifungua kwenye kituo hicho wataweza kupata malazi kwa wakati mmoja kwani kutakua na wodi 2.
Jengo la Maabara litaongeza huduma za uchunguzi wa kimaabara .
Nyumba ya mtumishi itaboresha mazingira ya mtumishi kufanya kazi kwenye mazingira rafiki hivyo huduma za dharura kupatikana kwa urahisi.
Kichomea taka kitasaidia usafi wa mazingira.
Jengo la kuhifadhia maiti litapunguza adha ya upatikanaji wa huduma ya kuifadhi maiti.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa